Mkenda: Nactvet nendeni na kasi ya mageuzi ya 4 ya viwanda

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameliagiza Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTVET) kuandaa semina na mafunzo ya kubadilisha uzoefu kila mwaka na nchi tofuati ili kuendana na kasi ya mageuzi ya nne ya viwanda ambayo yanahitaji ujuzi zaidi.

Mkenda ameyasema hayo leo Julai 14, 2023 katika semina ya kubadilisha uzoefu kwa viongozi wa vyuo vya elimu ya ufundi kutoka Tanznaia na China iliyofanyika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere Kibaha.

Aidha, Mkenda amesema, tayari serikali kupitia Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wamesaini makubalinao ya ushirikiano na Taasisi ya Ufundi ya  Chonqing (CQVIE) kutoka nchini China.

Miongoni mwa makubaliano ni  ushirikiano  baina ya Taasisi hizo  kubadilishana  uzoefu katika ujuzi wanaopata katika mafunzo kati ya Wanafunzi na Walimu (exchange program ).

Waziri Mkenda amesema ushirikiano huo umekuja wakati muafaka Tanzania ikiwa katika mchakato wa mageuzi  makubwa katika elimu.

“Tumeanzisha programu moja kati ya China na DIT, wanafunzi  wanasoma mwaka mmoja kisha miaka miwili wanaenda kusoka China, alafu mwaka wa mwisho wanakuja kumalizia nyumbani na kupata ‘degree’ yao.

“Kampuni ya Group six wamesema watawapatia kazi, tumeanza na wanafunzi 30 sasa hivi wapo ‘field’ (mafunzo kwa vitendo), tunataka kuongeza mashirikiano ili tuongeze idadi ya wanafunzi kwani  30 bado ni kidogo, pia  wakufunzi wao waje kufundisha wakufunzi wetu.

“Sisi ndio tungependa tuchague vyuo hivi vya kati vya mafunzo ya amali , ili tuweze kupata kile ambacho kitatusaidia kumove hapa tulipo.

“China imeendelea kwa sababu ya kutoa mafunzo kwenye vyuo vya kati, kuna wakati tulikuwa na kasi ya kila mmoja kuwa na elimu ya juu lakini kwa sasa mageuzi yetu ya elimu lazima yatoe a mafunzo ya amali.

Nae, Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dk Adolf Rutayuga amesema, semina hiyo imehusisha wadau wa vyuo 40 vya Tanzania na 30 vya China.

Amesema, “China wameendelea kwenye teknolojia hasa ya ujuzi, vijana kule wamekuwa chachu na msingi mzuri wa uchumi wa China, serikali yetu kuliona hilo wakatuagiza kuunganisha urafiki ili tubadilishane uzoefu.” Amesema Dk Rutayunga

“Tunataka vyuo vyote tuviunganishe na vya kule walimu na vijana wetu waende kule, na wao waje huku, ili vyuo vyetu vitoe vijana wenye ujuzi mahiri.”Amesema

Amesema, ujuzi kwa vijana utasaidia kutengeneza vitu vingi kwani vijana wa vyuo vyaa China wameunganishwa na viwanda  vitu vinavyozalishwa vinaingia sokoni moja kwa moja.

“Sasa  vyuo vyetu vinatokaje kwenye nadharia na kuingia sokoni moja kwa moja, ndio tunamekuja na huo mkakati wa kubadilishana uzoefu na kuwajengea ujuzi zaidi ili nao waweze kuzalisha vitu ambavyo vitaingia sokoni moja kwa moja,”amesisitiza.

 

 

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button