Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameutaka uongozi wa Bodi ya Huduma za Maktaba kusitisha ujenzi wa majengo na kujikita zaidi katika ununuzi wa vitabu mbalimbali vya maktaba.
Mkenda alitoa maagizo hayo jana, Julai 28, 2023 Jijini Dar es Salaam alipozungumza na menejimenti na watumishi wa bodi hiyo huku akisema kazi ya bodi hiyo ni kuhakikisha kunakuwa na maktaba zenye vitabu vya kutosha ambavyo vitawezesha watanzania kupata maarifa.
“Badala ya wekeza pesa nyinig katika ujenzi wa majengo nunueni vitabu na sambazeni katika maktaba zilizopo nchini ili kuwapa fursa watanzania kujisomea,” alisema waziri.
Aidha, alisema bodi hiyo inaweza kutafuta maeneo katika taasisi zikiwemo shule, vyuo vya maendeleo ya wananchi ama VETA vikatumika kama maktaba ambazo zitakuwa karibu na jamiii.
Comments are closed.