Mkojo wa sungura watumika kufukuza wadudu

Apigwa risasi akidhaniwa sungura

MKOJO wa sungura ukivundikwa kwa siku saba unaweza kutumika shambani kwa ajili ya kufukuza wadudu waharibifu kupitia harufu yake.

Ofisa kutoka Shirika la Agri Connect kwenye mradi unaosimamia na kutoa elimu ya kilimo cha mazao ya mbogamboga, matunda, kahawa na chai, Innocent Makura ameeleza hayo katika maonesho ya Nanenane kiitaifa yanayoendelea mkoani Mbeya.

Amesema mkojo huo wa sungura pia unatumika kama mbolea.

Advertisement

“Sasa kuna namna ya matumizi kama unataka utumie kama mbolea lita moja ya mkojo wa sungura unachanganya kwa lita 12 za maji hii inakuwa ni busta ambayo inafanya vizuri sana kwenye maharage na mazao mengine yote ya mboga mboga na matunda.

“Kwenye matunda ya muda mrefu unafanya vizuri sana kwenye parachichi na miembe,” amesema.

Amesema endapo mkulima atataka kutumia kama kiuatilifu cha kufukuza wadudu shambani, lita moja inachanganywa kwenye lita 15 za maji kwa hiyo harufu yake ile ndio inazuia wadudu wasiweke makazi shambani au kwenye mazao.

Vile vile nyama ya sungura ina protini nyingi kuliko nyama yoyote nyeupe ya mnyama wa nchi kavu.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *