Mkongwe Kombe la Dunia afariki
MKONGWE wa soka raia wa Mexico Antonio Carbajal, mwanasoka wa kwanza kucheza katika Kombe la Dunia matano, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93.
Carbajal raia wa Mexico anayejulikana kama El Cinco Copas baada ya mafanikio yake, alicheza Brazil 1950, Uswisi 1954, Sweden 1958, Chile 1962 na England 1966 Kombe la Dunia.
Carbajal alishikilia rekodi hiyo peke yake kwa miaka 32 hadi ilipofikiwa na Lothar Matthaus wa Ujerumani mwaka 1998.
Aliichezea nchi yake mechi 48, 11 kati ya hizo zilicheza Kombe la Dunia, pamoja na mechi 409 katika ngazi ya vilabu.
Sehemu kubwa ya uchezaji wake alizitumikia klabu ya Mexico ya Club Leon, ambapo alicheza michezo 364.
Klabu hiyo ilisema itafungua milango katika uwanja wake siku ya Alhamisi ili kuruhusu mashabiki kutoa heshima zao kwa “La Tota” pamoja na familia yake.
“Don Antonio, magwiji huwa hawafi,” klabu hiyo ilisema.”Siku zote tutafuata mkono wako.
Ni heshima kuwa timu yako.”