Mkongwe Zlatan aweka rekodi

MSHAMBULIAJI wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic amekuwa mfungaji mwenye umri mkubwa zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A.

Ibrahimovic, 41, alifunga bao la penalti katika mchezo wa ligi hiyo licha ya timu yake kupoteza mabao 3-1 dhidi ya Udinese jana.

Ibrahimovic aliisaidia Milan kushinda taji la Serie A msimu uliopita kabla ya kufanyiwa upasuaji majira ya joto kutokana na majeraha.

Hata hivyo, mkwaju wa penalti wa awali wa Ibrahimovic uliokolewa na kupigwa tena kufuatia baadhi ya wachezaji wa Udinese kuingia kwenye box kabla ya penalti hiyo kupigwa ambapo ni kinyume na sheria namba 14 ya upigaji wa penalti.

Bao hilo limemfanya mshambuliaji huyo, mwenye umri wa miaka 41 na siku 166, kupita rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Alessandro Costacurta (miaka 41, siku 25) kama mfungaji bora zaidi kuwahi kutokea kwenye ligi.

Habari Zifananazo

Back to top button