Mkubwa Fella: Miaka miwili tu inamtosha D Voice

MENEJA bora wa wasanii aliyeshinda washiriki kutoka nchi 58 kutoka kote duniani, Said Fella maarufu Mkubwa Fella amesema licha ya wengi kumbeza msanii aliyesajiliwa na Wasafi anawapa wadau hao miaka miwili tu msanii huyo atakuwa gumzo na mwenye mafanikio makubwa kupitia muziki wa singeli.

Anasema inawezekana wapo wasanii wenye uwezo mkubwa wa kuimba kuliko D Voice lakini wanamsaidia msanii huyo kutokana na kuwa na kipaji kikubwa kinachotaka nguvu kidogo kifikie mafanikio.

Advertisement

“Tumemchukua D Voice kutokana na uwezo mkubwa katika muziki anaofanya wa singeli lakini pia kupitia yeye tunataka kuupa thamani muziki wa singeli leo wanabeza lakini haitofika miaka hata miwili kupitia msanii huyu muziki wa singeli utapata thamani kubwa , atakuwa kioo cha mafanikio kwa wasanii wote wa singeli” anasema Mkubwa Fella.

Amesema wasanii wengi wa singeli hawapati shoo kubwa na muziki wao hauonekani kuwa na thamani kwa sababu wanakosa vitu vingi vikiwemo ‘connection’ na makampuni pamoja na wasanii wakubwa lakini kupitia D Voice nao watapata mwanga muziki wao utakavyokuwa nao watatamani kulipwa zaidi baada ya muziki wao kupanda thamani.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *