Mkulima wa mpunga asombwa na maji, afa

Mkulima wa mpunga asombwa na maji, afa

MKULIMA wa mpunga katika mtaa wa Nyampa, Kata ya Kasamwa wilayani Geita, Benjamin John, amefariki dunia baada ya kusombwa na maji ya Mto Nyampa alipokuwa akioga baada ya kutoka shambani.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Geita, Edward Lukuba amethibitisha tukio hilo na kueleza marehemu alizama na kusombwa na maji Desemba 28, 2022 majira ya saa mbili asubuhi.

Kamanda amesema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji walipokea taarifa hiyo majira ya saa sita mchana na kutuma askari kwa ajili ya kufanya utafutaji na uokoaji wa mwili,  lakini  hawakufanikiwa, hadi leo Desemba 29, 2022 walipoona mwili ukielea saa moja asubuhi.

Advertisement

“Katika tukio hili kulikuwa na ucheleweshaji wa taarifa, kwani tukio lilitokea jana (Desemba 28) majira ya saa mbili asubuhi, lakini taarifa kwa upande wa jeshi la zimamoto na uokojai zilikuja saa sita mchana, “ amesema.

/* */