Mkurugenzi Halmashauri Ngorongoro mambo safi

ARUSHA: Kamati ya siasa Mkoa wa Arusha ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Nassoro Shemzigwa kwa kukamilisha miradi iliyokuwa ikisuasusa awali likiwemo jengo jipya la ghorofa la ofisi za halmashauri ya wilaya hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa wilayani Ngorongoro wakati wa ukaguzi wa jengo hilo linalotumiwa na watumishi wa halmashauri huku ujenzi wake ukitengewa kiasi cha Sh bilioni 2.6.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo, Ofisa Mipango wa halmashauri hiyo,Emmy Hongoli amesema  mradi huo ulianza Machi, 2021 na unatarajia kukamilika Machi, 2024.

Amesema ujenzi huo unahusisha miundombinu ya ofisi za halmashauri,uzio,ujenzi wa nyumba za walinzi,nyumba ya kusambazia umeme, maegesho ya magari, barabara pamoja na taa za ulinzi.

“Mradi umekamilika kwa asilimia 95 lakini tunakabiliwa na mazingira magumu ya usafirishaji wa vifaa vya ujenzi hali inayopelekea kupunguza kasi ya utekelezaji wa mradi huu”

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Loy Thomas ole Sabaya  amempongeza Mkurugenzi wa halmshauri hiyo,  Shemzigwa  kwa kusimamia vema ujenzi wa jengo hilo ambali awali lilikuwa likisuasua kuendelea kwake.

Habari Zifananazo

Back to top button