Mkurugenzi kampuni ya kuzoa taka kortini

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzoa taka na usafi wa mazingira ya Together We Can Do Women Group ya jijini Arusha, Neema Mosha (39), mkazi wa Mtaa wa Moshono Kati, amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma kushindwa kuwasilisha Sh  milioni 49.

9 za jiji hilo.

Akisomewa mashitaka hayo leo na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mkoani Arusha, Rubein Maduhu,  ilidaiwa kuwa Mosha alitenda kosa hilo katika kipindi cha mwaka 2021/22, wakati kampuni hiyo ilipopewa uwakala wa kazi hiyo ya kuzoa taka na usafi wa mazingira.

Maduhu alidai hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Arusha, Regina Oyeri na kudai kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo wakati akijua wazi kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Mwendesha Mashitaka wa Takukuru alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo alimwomba Hakimu kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo, ambapo Hakimu Oyeri alipanga usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo kufanyika Machi 13, mwaka huu.

Habari Zifananazo

Back to top button