Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah ni miongoni mwa watu saba wa walioteuliwa kuwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo leo, Alhamisi, imetwataja wajumbe wengine wanaounda bodi hiyo kuwa ni mtangazaji wa zamani wa Shirika hilo, Amina Mollel, Cosmas Mwaisobwa, Innocent Mungy na Mwanjaa Lyezia.
Wengine ni Dr Hidelbrand Shayo pamoja na Justina Mashiba.
Mwenyekiti wa Bodi ya TBC, Mkurugenzi Mkuu, Menejimenti na Watumishi wamewapongeza wajumbe hao kwa uteuzi wao huku taarifa hiyo ikimalizia kwa kusema: “Tuna imani na usimamizi wa wajumbe hao, TBC itapiga hatua zaidi katika kukidhi mahitaji ya hadhira na wateja wake.”