Mkutano kilimo, teknolojia kuanza kesho Z’bar

ZANZIBAR; Mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu kilimo na teknolojia utafanyika kesho visiwani Zanzibar ukijadili uwekezaji katika sekta ya kilimo na Uchumi wa Buluu.

Mwanzilishi wa Taasisi ya KUA AFRIKA, Ahmed Aboutaleb amesema washiriki 100 kutoka Mataifa ya Afrika, Ulaya na Marekani watashiriki katika mkutano huo unaonza kesho na kumalizika keshokutwa.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Uvuvi Mifugo na Maliasili, Ali Khamis anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo.

Habari Zifananazo

Back to top button