Mkutano mapambano ya rushwa Afrika waiva

TANZANIA itakuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa maadhimisho ya siku ya mapambano dhidi ya rushwa barani Afrika, utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kuanzia Julai 9-11, 2023.

Hayo yamebainishwa  leo jijini Dar es Salaam  na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini -Takukuru, Doreen Kapwani na kusema kuwa maadhimisho hayo maandalizi yake wameshirikiana  na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA).

Amesema Jumapili ya wiki hii, Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi atazindua maadhimisho hayo na siku ya kilele chake Jumanne itakuwa Julai 11, ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

“Maadhimisho haya ni ya kila mwaka ambapo zinakusanyika mmlaka zote za kupambana na rushwa barani Afrika, ili kufanya tathimini ya mafanikio na changamoto ya Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa mwaka 2003 unaofikisha umri wa miaka 20 kwa sasa,” amesema Doreen.

Amesema maadhimisho hayo yataambatana na shughuli mbalimbali, ikiwemo   matembezi ya amani ya mapambano dhidi ya rushwa siku ya uzinduzi  yatakayoanzia  ofisi ya Mkuu wa Mkoa  na kuishia AICC.

Pia amesema kutakuwa na idahalo mbalimbali kutoka kwa wakuu wa mamlaka za kuzuia rushwa barani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wanasiasa,vijana na viongozi wa dini.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button