Mkuu wa kituo cha polisi Chiungutwa afariki
MKUU wa kituo kidogo cha polisi Chiungutwa wilayani Masasi mkoani Mtwara amefariki dunia baada ya kupigwa risasi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katemba ametoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ambapo amesema askari huyo amefariki Februari 1 mwaka huu mchana katika Hospitali ya Ndanda wilayani humo.
Amemtaja kwa majini marehemu huyo kuwa ni A/INSP Eliuterius Hyera aliyefariki akiwa anaendelea na matibabu hospitalini hapo.
Amesema marehemu huyo akiwa ameongozana na askari mwenzake katika ukamataji wa watuhumiwa wa tukio la kuvunja ofisi na kuiba ambapo mtuhumiwa alianza kukimbia ili asikamatwe.
Kitendo cha mtuhumiwa huyo kukimbia ndipo askali aliyekuwa na bastola alipofyatua risasi kwa lengo la kufanikisha ukamataji na ikapelekea kumjeruhi mkaguzuzi huyo.
‘’Juhudi za kuokoa maisha yake zilifanyika kwa kupelekwa hospitali ya ndanda ambako alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu na mwili umehifadhiwa hospitalini hapo kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa anashikiliwa kwa hatua zaidi za kisheria’’amesema Katembo
Hata hivyo juhudi za kuwasaka watu waliyohusika katika tukio hilo zinaendelea kufanyika ili kuweza kuwafikisha mbele ya sheria.
‘’Marehemu amepoteza damu nyingi sana kwa kuwa jeraha lilikuwa mbele ya kifua na nyuma sehemu ya mgongoni kwahiyo kifo kimesababishwa na upotevu mwingi wa damu’’amesema Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Shayo Mganga