HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili(MNH), imetangaza kufunga lango kuu la kuingilia kwa waenda kwa miguu kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Desemba 12 ,2022, hadi Machi 30,2023, ili kupisha ukarabati wa eneo hilo.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu Kitengo cha Uhusiano wa Hospitali hiyo, Neema Mwangomo, imesema kufuatia hatua hiyo, wananchi watakaofika hospitalini wanashauriwa kutumia geti la kutokea lililokaribu na jengo la wazazi.
“Tunapenda kuwatangazia wananchi wote kwamba tunafunga lango kuu la kuingilia hospitali kwa waenda kwa miguu kwa miezi mitatu,”amesema.
Mwangomo ameeleza kuwa wananchi pia watatakiwa kutumia geti la kuingia chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), lakini wanaotumia magari kuingia hawataathirika na ufungaji huo.
“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza ,tunaomba ushirikiano wenu ,”amesisitiza