Mlinzi kizimbani akidaiwa kunajisi mtoto

MKAZI wa Kata ya Nzovwe, jijini Mbeya, Isaya Nswila  (36) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya akidaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 12.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Emanuel Bashome, mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi, Paul Ntumo alidai kuwa Nswila ambaye ni mlinzi wa kampuni mkoani Mbeya, alitenda tukio hilo kati ya Januari Mosi 2022 hadi Novemba 30 katika eneo la Nzovwe jijini Mbeya kwa kumbaka mtoto huyo.

Bushome alidai kuwa kitendo hicho ni kinyume na kifungu namba 130 (1) (2) e na kifungu namba 131 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Advertisement

Mshtakiwa alikana kuhusika na upande wa Jamhuri uliieleza mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Hakimu Mkuu Mwandamizi, Ntumo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 17 mwaka huu.