Mlipuko lori la mafuta 40 wafa Liberia

TAKRIBAN watu 40 wamekufa kufuatia mlipuko wa lori la gesi Kaskazini mwa Liberia, ofisa mkuu wa matibabu, Francis Kateh, amesema.

Lori la mafuta lilianguka Jumanne jioni huko Totota, Kaunti ya Lower Bong, na baada ya kulipuka liliuwa na kujeruhi watu wengi waliomiminika eneo la tukio.

“Makumi ya watu bado wako hospitalini wakiwa wameungua vibaya, na idadi ya vifo inaweza kuongezeka.” Kateh alisema.

Habari Zifananazo

Back to top button