DODOMA: UONGOZI wa Mkoa wa Dodoma umetangaza mlipuko wa ugonjwa wa surua katika mkoa huo na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,Patrick Bashemara amesema mlipuko wa ugonjwa huo wa surua umebaini baada ya sampuli zilizochukuliwa kuthibitika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Surua.
“Kwa barua hii mnaelekezwa kuwajulisha wananchi kuchukua tahadhari juu ya mlipuko wa ugonjwa wa surua na pia kuwapeleka watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika Zahanati au vituo vya afya kupatiwa chanjo ya ugonjwa huo.
Comments are closed.