Mloganzila kupandikizaji nyonga, magoti bandia
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila itafanya kambi maalumu ya upasuaji wa kuweka nyonga na magoti bandia kwa wagonjwa wenye changamoto ya nyonga na magoti.
Upasuaji huo utafanyika kwa kushirikiana na Hospitali ya Queen Elizabeth ya nchini Uingereza kuanzia Novemba 27 hadi Disemba 1,2023.
Daktari bingwa wa upasuaji mifupa, nyonga na magoti, Dk. Shilekirwa Makira amesema wagonjwa watakaonufaika na huduma hizo ni pamoja na wenye matatizo ya nyonga zilizosagika zenye maumivu makali na magoti yaliyosagika.
Dk Makira ameongeza kuwa watu wenye changamoto hizo watabadilishiwa kwa kuwekewa nyonga na magoti bandia kitu kitakachowafanya waondokane na maumivu wanayoyapata kabla ya nyonga zao kubadilishwa.