Mmiliki kiwanda cha pombe awasilisha ombi kwa Waziri Kijaji

MAFANYABIASHA maarufu katika mji wa Namanga wilayani Longido mkoani Arusha, Dalton Karago  anayemiliki Kiwanda cha kutengeneza Pombe kali cha Dalton’s Beverage amemuomba Waziri wa Biashara na Viwanda, Ashatu Kijaji kuingilia kati hatua ya Mkuu wa Wilaya ya Longido, Marco Ng’umbi ya kukifungia kiwanda chake wakati anavibali vyote vya serikali vya kuanzishwa kwa kiwanda hicho.

Karago alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari katika na kusema madai ya Mkuu wa Wilaya Ng’umbi kuwa kiwanda chake ni bubu sio wa kweli kwani ana vibali vyote halali vya vya kuanzishwa kwa kiwanda hicho alivyopewa na idara za serikali.

Karago alisema kauli ya kukitangaza kiwanda chake ni bubu kimemdhalilisha yeye binafsi, jamii iliyomzunguka na wafanyabiashara na wateja wake wengi wamekuwa hawana imani na yeye na kuonekana anatengeneza vitu feki wakati sio kweli.

Alisema kwa kauli hiyo ameomba kumuona Waziri Kijaji kuingilia kati suala hilo ili aweze kufunguliwa kiwanda chake kwani uamuzi wa kufungiwa kiwanda chake tangu Agosti 24 mwaka huu ni uonevu na kibaya zaidi wafanyakazi wake waliwekwa rumande kituo cha Polisi Longido kwa siku 16 bila sababu na sababu zilizotolewa na Mkuu wa Wilaya hazina uthibitisho wowote kuwa Kiwanda hicho ni bubu.

Alisema alifuata taratibu zote za kuanzishwa kwa kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na kukaguliwa na kupata kibali Shirika la Viwango Tanzania (TBS), leseni ya biashara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Longido, uthibitisho wa ulipaji kodi (TIN) usajili Brela wa kampuni Dalton’s Beberage na usajili wa majina ya vinywaji vya Wasafi Banana na Wasafi Vodka & Gin toka Brelana.

Baada ya hapo kulikaguliwa na Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo Nchini (SIDO) na kupewa barua ya uthibitisho wa uhalali wa kiwanda hicho.

Mkurugenzi huyo wa Dalton’s Beberage alisema kuwa Novemba 23 mwaka jana mtendaji wa kata ya Namanga alimwandikia nakala ya barua Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Longido ya kumtambulisha kuwa kuna kiwanda cha pombe kali na pia kumtaka meneja huyo kumpatia stika ili aweze kufanya shughuli za kibiashara ikiwa ni pamoja na kulipa kodi stahiki za serikali.

Alisema na kusikitishwa na kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Longido ya kuambiwa kuwa kiwanda chake cha Dalton’s Bevarage ni kiwanda Bubu wakati kauli hiyo sio ya kweli na imemwomba Waziri kuliangalia suala hilo kwa jicho la tatu.

Karago alisema kuwa maslahi ya wafanyabiashara wadogo wenye nia ya kujiajili na kukikomboa lakini kuna baadhi ya watendaji wa serikali wanakwamisha jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kutaka vijana kuacha kuwa ombaomba na kujiajili kwa kuanzisha viwanda kwa kufuata masharti yote ya serikali.

‘’Nakuomba Waziri Ashatu Kijaji nimeonewa kwa kufungiwa kiwanda change njoo ujue ukweli na hadi sasa nimepata hasara kubwa sana toka kiwanda change kilipofungwa ‘’alisema Karago

Akizungumzia tuhuma hizo Mkuu wa Wilaya ya Longido Marco Ng’umbi alisema kuwa amekifungia kiwanda cha kutengeneza pombe kali cha Dalton’s Beverage kilichopo Mtaa Saba kata ya Namanga wilayani humo kwa madai kuwa kiwanda hicho ni bubu na kusema amewaweka wafanyakazi wa kiwanda hicho siku 16 sio ya kweli.

Ng’umbi alisema kuwa mtazamo na mwelekeo wa Wilaya ya Longido ni kuvutia wawekezaji wakubwa,wadogo na wakati na wote wanapaswa kufuata sheria za serikali.

Ng’umbi alisema iwapo mwekezaji atafuata sheria za uwekezaji katika Wilaya ya Longido kamwe hawezi kusumbuliwa lakini asiyefuata sheria hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake bila kujali ukubwa wake au uhusiano wake na jamii.

Alisema mmiliki wa kiwanda hicho ameajili wafanyakazi wa nje bila ya kuwa na kibali na pia amefanya eneo la kiwanda kama sehemu ya kuhifadhi madawa ya kulevya hivyo hatua zaidi zimechukuliwa dhidi yake kwa kukifungia.

 

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button