Mmoja apoteza maisha 15 wajeruhiwa ajali Kamata ‘DSM’

MTU mmoja amepoteza maisha na wengine 15 kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha treni na daladala yenye namba za usajili T710 DKJ aina ya ‘Eicher’ linalofanya safari zake kati ya Kigamboni na Machinga Complex katika eneo la Kamata Kariakoo Dar es Salaam leo Alhamisi Mei 18, 2023.
 
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli Tanzania, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa majeruhi wamewahishwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili huku mwanamke mmoja akiwa Moi baada ya kukatika mkono.
 
ACP Mbuta amesema chanzo cha ajali hiyo ni ubishi wa devera wa gari hiyo ambaye amekimbia baada ya ajali, aliyelazimisha kuvuka bila kuangalia pande mbili na kupinga agizo la kusimama la mshika kibendera wa reli.
/* */