Mmoja auawa DRC mapigano ya jeshi na M23

DRC: Mapambano yamezuka Kati ya Jeshi la FARDC na kundi la M23, wilayani Rutshuru Kaskazini mwa Jimbo la Kivu, imeripotiwa kuwa mapambano hayo yameingia siku ya pili hii leo.
Habari za kuaminika zinaeleza kuwa wanajeshi wa Kongo wamedhibiti vijiji wilayani Rutshuru leo saa tatu asubuhi.
Vita hiyo imepiganwa kwenye kijiji cha Bambo ,Chefferiani Bwito, watu wawili wamejeruhiwa vikali, na mmoja kufariki kutokana na bomu lilopigwa na waasi wa kundi la M23 wakipewa nguvu na Serikali ya Rwanda.

Habari Zifananazo

Back to top button