Mnyama amuita Azam Kirumba

DAR ES SALAAM: KLABU ya @simbasctanzania itautumia Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya @azamfcofficial utakaopigwa Februari 09, 2024.
Mchezo huo wa kiporo uliacha maswali mengi, ni wapi utafanyika baada ya Viwanja vya Uhuru na Benjamini Mkapa Dar es Salaam kufungwa kwa muda kupisha ukarabati unaoendelea.
Juhudi za Viongozi wa Simba kutafuta uwanja mbadala zilikumbana na changamoto baada ya maombi ya kutumia Uwanja wa New Amaan complex wa visiwani Zanzibar, kugonga mwamba.
Sasa ni rasmi mchezo huo utapigwa Uwanja wa CCM Kirumba, hii inakuja baada ya Azam Fc kuchapisha taarifa katika mitandao yake kuwa mtanange huo utapigwa Februari 09 dimbani hapo.

Habari Zifananazo

Back to top button