DAR ES SALAAM: Klabu ya Simba leo inatupa karata yake nyingine katika Ligi Kuu huku hesabu zikiwa ni kupunguza tofauti ya alama dhidi ya Yanga pamoja na Azam Fc.
Leo usiku Simba watakuwa Uwanja wa Azam Complex kuwavaa Mashujaa ya Kigoma. Kocha msaidizi wa timu hiyo Seleman Matola amesisitiza kuwa michezo iliyosalia ina umuhimu mkubwa kwani kila timu inataka kujiweka kwenye mazingira bora zaidi.
“Ligi inaelekea ukingoni, kila timu inataka kuondoka nafasi iliyopo ili kujiweka nafasi nzuri zaidi, tunategemea upinzani lakini tumejipanga” alisema Matola alipozungumzia utayari wa kikosi hicho kuivaa Mashujaa leo.
Simba mpaka sasa imejikusanyia alama 42 katika michezo 18 iliyoshuka dimbani alama 10 nyuma ya vinara Yanga.