Mo Dewji amteua Magori kuwa mshauri wake Simba

Rais wa heshima wa klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji amemteua Crescentius Magori kuwa mshauri wake ndani ya klabu hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mo Dewji amesema ameamua kufanya uteuzi huo baada ya kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na kiongozi huyo ndani ya Simba SC.

“Kufuatia kazi nzuri aliyoifanya Ndugu Crescentius Magori katika kunishauri kuhusu maendeleo ya Klabu yetu ya Simba, nimeteua tena kwa kipindi kingine kuwa Mshauri wangu kuhusu michezo kwa ujumla na maendeleo ya Klabu.” Amesema Mo Dewji.

Novemba 4, 2018, Magori alitangazwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo, Juni 13, 2029 aliiandikia barua Bodi ya Wakurugenzi ya kujiuzulu kabla ya mchakato wa kumpata CEO mpya ambapo nafasi hiyo ilichukuliwa na Barbara Gonzalenzi aliyejiuzulu hivi karibuni.

Habari Zifananazo

Back to top button