MOI kunufaisha wagonjwa wa vibiongo zaidi ya 50

DAR ES SALAAM: Zaidi ya Watanzania 50 wenye matatizo ya vibiongo wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji kupitia kambi ya matibabu na mafunzo inayo endelea katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) ikihusisha madaktari kutoka ndani na nje ya nchi.

Hayo yametanabahishwa leo Februari 9, 2024 wakati wa mafunzo katika Kambi ya matibabu na mafunzo katika taasisi hiyo.

Kaimu Mkurugenzi katika taaisisi hiyo, Dk Laurent Lemely amesema wagonjwa wa vibiongo wanaendelea kuongezeka nchini hadi kufika wagonjwa watatu kwa mwezi huku takwimu za dunia ikiwa ni asilimia 1 na kwa wiki hii jumla ya Watanzania 10 watafanyiwa upasuaji.

Pia, madaktari wanaotoa mafunzo hayo kutoka Nchini Italia na Uingereza wamesema nia ya kuendesha mafunzo hayo ni kutaka kuongeza uwezo wa madaktari wa kitanzania katika matibabu ya vibiongo na pasuaji nyingine ngumu ili kuboresha sekta ya Afya Tanzania

Kwa upande mwingine, Madaktari Watanzania wanaoshiriki katika mafunzo hayo wamesema programu hiyo itawezesha kuendelea kutoa matibabu ya kibingwa hasa ya vibiongo ambayo wagonjwa wake wanatajwa kuongezea kwa kasi.

Kambi hiyo imeanza tangu mwaka 2019 ambapo imekuwa ikifanyika kwa kuangalaia matibabu mbalimbali husuasani yale ya kibingwa ili kuongeza uwezo wa madaktari wa kitanzania

Habari Zifananazo

Back to top button