Monalisa aja na Usiku wa Tuzo za Wanawake

DSM; Msanii mkongwe wa filamu nchini Yvone Cherrie ‘Monalisa’ , ameandaa Usiku wa Tuzo za Wanawake Novemba 23 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Monalisa amesema zitafanyika ukumbi wa Super Dome Masaki na kwamba ni nafasi ya wanawake kuonekana kwa kile wanachofanya.

“Nimeandaa tuzo za wanawake vinara kwenye sekta ya sanaa, michezo na habari,  ili kuwapa chachu wanawake kufanya vizuri zaidi ya wanavyofanya,” amesema.

Amesema kuwa tuzo hizo zitatolewa kwa mwanamke bora kwenye michezo, habari, washehereshaji na sanaa za mikono.

“Wanafanya vitu vikubwa lakini hawapati nafasi ya kujulikana katika jamii kutokana na wanachokifanya, unachotakiwa ni kumpendekeza mwanamke unayeona anastahili kupata tuzo kutakuwa na majaji watamchagua kutokana na kazi yake, “amesema Monalisa.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button