Monalisa ashinda tuzo kimataifa

MWIGIZAJI Mtanzania Yvonne Cherrie, maarufu kama ‘Monalisa’ ameshinda tuzo ya kimataifa Emmy Kids 2022 katika series ya ‘My Better World Show’ kwa kuingiza sauti kwa lugha ya Kiingereza.

Baada ya ushindi huo, Monalisa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ameandika “Miaka minne iliyopita, nilikuwa mmoja wa waigizaji tuliochaguliwa kuingiza sauti kwa lugha ya Kiingereza katika series ya My Better World Show ambapo mimi binafsi nilitia sauti ya wahusika watatu…

…Napenda kukujulisha kuwa, series hiyo imeshinda moja kati ya tuzo kubwa sana duniani, tuzo za EMMYS 2022, katika Kipengele cha International Emmy Kids: Entertainment and Factual. Na usiku wa jana tulipata wasaa wa kukutana CAST and CREW ili kusherehekea ushindi huo.”ameandika Monalisa.

Amemaliza kwa kuandika “Sio mbaya ukaanza kuniita Emmy award winner voice over artist. Hongera kwa Timu nzima kwakweli, maana ni kazi kubwa iliyoshirikisha watu mbalimbali wa nchi mbalimbali za Afrika.”

Habari Zifananazo

Back to top button