Moni: Nahisi kukata tamaa

MSANII wa Hiphop Moni Centrozone ameeleza hisia za kufikia hatua ya kukata tamaa kutokana na changamoto anazopitia ikiwemo kutosaidiwa kimuziki hali inayofanya ashindwe kufikia ndoto zake.
Moni amesema licha ya juhudi kubwa, nidhamu aliyonayo, lakini kuna wakati watu wake wa karibu hawamuungi mkono na kwamba pengine watu hao wanaona hastahili kuwa kwenye nafasi aliyopo kwa sasa.
“Kuna naona wenzangu wanavopata ‘treatment’ (kuungwa mkono) lakini mimi nimekuwa nikipambana bila kukata tamaa bila mikwaruzo na wasanii wenzangu ambao ni ndugu zangu lakini tunashindanishwa kichini chini na aslimia kubwa wanaochangia kwenye hizi fitna ni kwenye familia humu humu ndani yetu,” amesema Moni.
Moni amesema ndoto yake kwa sasa ni kuachia albamu, lakini baadhi ya watu wanamshauri kutoa albamu hiyo kikubwa kwa maana atumie pesa nyingi kufanya ziara, uzinduzi na matangazo “vitu ambavyo vinagarimu sana na kuna wenzangu wanafanya na wanasapotiwa lakini kwangu hakuna.” ameandika Moni Instagram.
Kutokana na changamoto hizo, Moni ameeleza kuhisi kubagulia na wakati mwingine hata kukosa mialiko ya wasanii wenzake “yote haya ni kutoka moyoni hata ikitokea leo nimekufa nisife na vitu moyoni.” amemaliza kwa kutoka hisia kali.