Moro wakusanya mapato kwa 100%

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imefanikiwa kufi kia lengo kwa kukusanya mapato ya ndani ya Sh bilioni 12 .653 ambayo ni sawa na asilimia 100 ya makisio yaliyowekwa ya Sh bilioni 12.654 mwaka wa fedha 2022 /23.

Meya wa Manispaa hiyo, Pascal Kihanga alisema hayo mjini Morogoro katika mkutano wa kawaida wa mwaka wa Baraza la Madiwani wa halmashauri manispaa hiyo. Kihanga alisema manispaa imeweka mikakati ya kuongeza kukusanya mapato kwa mwaka wa fedha wa 2023/24.

Alitaja mikakati hiyo ni pamoja na utoaji elimu kwa walipakodi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na ushuru kwa ustawi wa maendeleo ya wananchi na kikosi kazi maalumu cha ufuatiliaji wa mapato ambacho kimeanza eneo la Msamvu.

Kihanga alisema katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, serikali kuu imetoa jumla ya Sh bilioni 8.497 ambazo ni saw ana asilimia 93 ya makisio ya Sh bilioni 9.115 ya mwaka wa fedha 2022/23.

Alisema miongoni mwa fedha hizo sh bilioni moja ni ujenzi wa Hospitali ya wilaya kwa kujengwa majengo manne ambayo ni wodi ya wazazi, mionzi, kufulia, jengo la dawa ambayo yapo yapo hatua za umaliziaji.

Kihanga alisema sehemu nyingine ya Sh milioni 50 zimetumika ujenzi wa wodi ya wazazi kwenye Zahanati ya Konga ambapo jengo hilo lipo hatua ya umaliziaji. Katika hatua nyingine alisema, Manispaa imetumia Sh milioni 555 ambazo ni sehemu ya mapato ya ndani kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa kituo cha afya kimoja na zahanati nne ndani ya manispaa hiyo.

Dwani wa Kata Mindu, Zuber Mkalaboko alichangia hoja mapato aliishauri Menejimeti ya Manispaa kuandaa mikataba inayoziba mianya ya kuzalisha madeni dhidi ya wapangaji.

Pia kutumia mifumo ya kielektroniki ya tehama katika uendeshaji wa vitenga uchumi vya Manispaa ili kudhibiti masuala ya rushwa, upendeleo na uzalishaji wa madeni.

Diwani wa kata ya Mafisa, Joel Kisome alisema bado Manispaa inapoteza mapato kwa sababu ya usimamizi usiofaa unaoweka vigezo wapangaji mpya kulipa madeni ya nyuma kabla ya kukabidhiwa vyumba vya biashara Kisome alitoa mfano katika kituo cha mabasi cha Msamvu vyumba vingi vya biashara vimefungwa kwa kukosa wapangaji wapya licha uhitaji mkubwa kutokana na masharti yaliyowekwa jambo ambalo hawajibiki nalo.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button