Moto waua 14 Vietnam

MOTO uliozuka katika jengo la makazi katika mji mkuu wa Vietnam, Hanoi umesababisha vifo vya watu 14 na kujeruhi wengine watatu, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Moto huo umeelezwa ulianza katika jengo la ghorofa tano katika eneo la Cau Giay katikati mwa Hanoi majira ya saa 12:30 asubuhi leo, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.

Moto huo mkubwa umeelezwa kwamba ulikuwa ukiwaka huku ukitoa milipuko kadhaa, Shirika la Habari la Vietnam (VNA) limeeleza.

Wizara ya Usalama wa Umma ya Vietnam imesema kwamba wazima moto waliwaokoa watu saba kutoka kwenye jengo hilo baada ya kufanikiwa kuuzima moto huo.

Inadhaniwa kuwa motohuo ulianza katika ua kati ya vitalu viwili vinavyotumiwa kuuza na kurekebisha baiskeli za umeme, ingawa maofisa wa serikali wanachunguza chanzo cha moto huo na bado hawajatambua idadi ya wanaohisiwa kufa katika ajali hiyo.

Kulingana na taarifa za Wizara ya Usalama wa Umma, kati ya mwaka 2017 na 2022, watu 433 walikufa katika moto uliounguza nyumba 17,000 nchini humo, wengi wao wakiwa katika maeneo ya mijini,

Mwezi Septemba, watu 56 wakiwemo watoto wanne walikufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika moto uliotokea katika jengo moja la makazi mjini Hanoi.

Mnamo mwaka wa 2022, watu 32 walikufa katika Baa ya Karaoke iliyojaa watu wengi kusini mwa Vietnam, huko Thuan An kutokana na moto uliosababishwa na nyaya fupi ya umeme.

Habari Zifananazo

Back to top button