Moto waua 40 Chile

CHILE: SERIKALI ya Chile imetangaza hali ya hatari huku ikiendelea kupambana na moto mkali wa uliozuka katika moja ya msitu katikati mwa nchi hiyo, ambao hadi sasa umeua takribani watu 40.

Rais wa Chile, Gabriel Boric amesema hapo jana kwamba takribani watu 40 wamekufa na kuonya kwamba idadi ya vifo huenda ikaongezeka.

“Watu wengine sita wako hospitalini kwa sababu ya majeraha ya moto,”

“Vikosi vyote vimetumwa katika mapambano dhidi ya moto huo,” Boric alisema katika chapisho la awali kwenye mtandao wa X alipokuwa akisema huduma za dharura zinakutana kutathmini hali hiyo.

Moto huo umeteketeza maelfu ya hekta za misitu tangu Ijumaa, ukiifunika miji ya Pwani na kuwalazimu watu kukimbia makazi yao katika maeneo ya kati ya Vina del Mar na Valparaiso.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Carolina Toha awali alisema kuwa timu za uokoaji zilikuwa zikitafuta maeneo yaliyoathiriwa.

Habari Zifananazo

Back to top button