Moto wauwa watoto hospitalini India

Mmili wa hospitali awakimbia polisi

NEW DELHI, India: WATOTO saba waliozaliwa hivi karibuni wamefariki dunia katika ajali ya moto uliotokea katika hospitali ya watoto katika Mji Mkuu wa India, New Delhi saa chache baada ya moto mwingine kuzuka katika katika eneo la burudani la familia katika Wilaya ya Rajkot ya Gujarat na kuua watu kadhaa.

Afisa wa uokozi wa majanga ya moto katika eneo hilo, Atul Garg akizungumza na vyombo vya habari vya nchini humo ameeleza kuwa waokoaji waliwachukua watoto 12 kutoka hospitalini hapo hadi kituo kingine, lakini watano kati yao walikufa kutokana na moshi.

Garg amesema watoto watano waliokolewa na wanatibiwa baada ya kuvuta moshi mwingi.

Moto huo ulitokea usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya watoto katika eneo la Vivek Vihar mjini New Delhi.

Soma pia: https://habarileo.co.tz/moto-wateketeza-vibanda-vya-biashara-kigoma/

Suresh Kumar, afisa mwingine wa uokoaji wa majanga ya moto, amesema moto huo ulizimwa kwa takriban saa moja na sababu ya kutokea kwake bado inachunguzwa.

Afisa wa polisi, Surendra Choudhary katika taarifa yake amesema walipofika hospitalini hapo, watoto kadhaa walikuwa wamekufa lakini watoto wote 12 waliozaliwa hivi karibuni waliokolewa kutoka hospitali hiyo kwa msaada wa watu wengine.

Mmiliki wa hospitali hiyo amekimbia. Polisi wamesema wanamsaka ili achukuliwe hatua za kisheria.

Waziri Mkuu wa Delhi, Arvind Kejriwal aliliita tukio hilo kuwa la kuvunja moyo.

“Sisi sote tuko pamoja na wale waliopoteza watoto wao wasio na hatia katika ajali hii,” ameandika waziri huyo kwenye ukurasa wake wa X.

Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7b0xAguZu3/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

Tukio lingine la moto limetokea saa chache huko nchini India ambapo watu zaidi ya 20 wamepoteza maisha wakiwemo watoto 9 katika moto mkubwa uliotokea katika bustani ya burudani ya Rajkot katika jimbo la magharibi la Gujarat.

Watu wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo, ripoti za vyombo vya habari vya eneo hilo zimeeleza hayo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button