Moto wazuka Mwananchi Communications

DAR ES SALAAM: Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) imesema hakuna aliyeumia wakati wa tukio la moto lililozuka katika stoo za kampuni hiyo yenye makao makuu yake Tabata Relini jijini Dar es Salaam.

Bakari Machumu, Mkurugenzi Mtendaji wa MCL amesema moto huo ulidhibitiwa haraka na chanzo cha moto huo hakijulikani wakati huu. 

“Kipaumbele chetu kwa sasa ni usalama wa wafanyakazi wetu na kuilinda jamii inayotuzunguka. MCL inadhamiria kuendelea kuhakikisha usalama na ustawi wa watu wake. Uchunguzi unaendelea, na tutaweletea taarifa zaidi pindi utakapokamilika,” amesema Machumu akisisitiza kuwa biashara na shughuli za katika kampuni hiyo zilikuwa zinaendelea.

Habari Zifananazo

Back to top button