Mount akaribia Old Trafford

KIUNGO mshambuliaji wa Chelsea, Mason Mount anafanyiwa vipimo vya afya muda huu katika uwanja wa mazoezi wa Carrington kwa ajili ya kujiunga na Manchester United.

Taarifa iliyotolewa na mwandishi wa habari za michezo nchini Italia, Fabrizio Romano imeeleza kuwa Mwingereza huyo atasaini mkataba wa miaka mitano utakaomuweka Old Trafford hadi mwaka 2028 wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja mpaka Juni 2029.

United inapanga kumtangaza mchezaji huyo kama usajili wao kwanza mara baada ya vipimo na mipango ya mwisho kwenda sawa.

Mount atakamilisha dili huo kwa ada ya uhamisho wa £55m pamoja na ongezeko la £5m.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button