Mourinho:Nilipata kazi timu ya taifa, Madrid waligoma

KOCHA wa zamani wa AS Roma Jose Mourinho, ameweka wazi kwamba aliwahi kupata nafasi ya kufundisha timu ya Taifa ya Ureno lakini uongozi wa timu ya Real Madrid ulimzuia.

Morinho anayefahamikwa kwa jina la ‘Special One’ alibainisha hayo katika mahojiano na TribalFootball, ambapo amesema kuwa Ureno ilimpa kazi mara mbili lakini kipindi hicho Real Madrid ilikuwa katika mashindano makubwa hivyo haikukubali kumuachia.

“Nilikuwa na nafasi ya kuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Ureno, nilipata nafasi mara mbili. “Mara ya kwanza nilipokuwa Real Madrid lakini Florentino Perez aliniambia, ‘hakuna nafasi’. “Mara ya pili nilikuwa Roma, nilifutwa kazi miezi michache baadaye … lakini sijutii,” Mourinho alisema mapema wiki hii: “Nataka kufanya kazi msimu wa joto.” Mourinho.

Advertisement

Mreno huyo mwenye miaka 64, amekuwa nje ya kazi ya ualimu wa mpira tangu alipotimuliwa na timu ya  AS Roma ya nchini Italia mwezi Januari mwaka huu.

“Kufundisha timu ya taifa ni lengo kwangu,” amesema Mourinho. “Labda kabla ya Kombe la Dunia, Euro au Copa America na Kombe la Afrika ntakuwa mwalimu wa moja ya timu. Naweza, ndiyo. Nimesubiri kwa miaka miwili nikiwa nje ya kazi yangu ya ualimu wa soka huenda siku moja ikatokea hilo.” Ameeleza Mourinho.

Pia Mourinho amewahi kuifundisha Chelsea, Manchester United na Tottenham katika Ligi Kuu ya England, Real Madrid ligi ya Uhispania, Inter Milan ya Italia na FC Porto ya Ureno.