Mpanda kujenga madarasa 51 sekondari

HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi, imepokea kiasi cha Sh bilioni 1.02, kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 51 katika shule zake zote za sekondari.

Akisoma taarifa mbele ya baraza maalumu la madiwani wa halmashauri hiyo, Mkugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Sophia Kumbuli ,amesema ujenzi wa madarasa hayo utawezesha wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani kuanza masomo kwa pamoja.

Katika hatua nyingine Kumbuli, amesema halmashauri hiyo imetenga kiasi cha zaidi ya Sh bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule za msingi.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph amewataka wataalamu wa halmashauri hiyo kuhakikisha madarasa hayo yanakamilika kabla ya msimu wa masika kuanza, huku akisisitiza usimamizi utakaoonesha thamani ya fedha.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x