Mpango: Chukieni rushwa

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amesisitiza ni wajibu wa kila Mtanzania kuchukia rushwa

Mpango amesema ni wajibu kila mtu kuyaishi maisha ya Hayati Rais Mwalimu Julius Nyerere ambaye alichukia vitendo vya rushwa.

Dk Mpango ametoa kauli hiyo leo Oktoba 14 wakati wa Misa maalum ya kumuombea Hayati Mwalimu Julius Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Babati mkoani Manyara.

“Mwalimu Nyerere alikuwa mkweli na hakupenda fitina, kwahiyo nasi tujitahidi sana kukwepa kuwa wafitini.

” amsema Dk Philip Mpango.

Habari Zifananazo

Back to top button