NIC Insurance katika kuboresha huduma zao na kuwarahisishia wananchi kujiunga na bima, wamekuja na ‘bima kiganjani’ ambayo mwananchi yoyote anaweza kuikata mwenyewe popote alipo na kwa wakati wowote.
Afisa Tehama wa NIC Ablafizi Kibiki amesema watanzania wataweza kutumia huduma ya bima kidigitali na kuokoa muda ambao mtu angeutumia kwenda kwenye ofisi hizo kukata bima.
“Tuna NIC kiganjani ambayo ni ‘App’ mtu anaipakua kutoka ‘play store’ na itampa maelekezo yote namna ya kujisajili, ipo kwa lugha zote mbili Kiswahili na Kingereza.”Amesema Kibiki na kuongeza
“ Kupitia NIC kiganjani mteja ataweza kupata huduma zote muhimu na vifurushi vyote vya bima ambavyo anahitaji na kujisajili.
Amesema, NIC kiganjani inamfikia mtanzania yeyote hata ambao wapo nje ya Tanzania na huduma hiyo mtu ataipata hata akiwa chumbani amelala akihitaji kufuatilia madai.
Comments are closed.