Mpogolo aweka mkazo amani Ilala

DAR ES SALAAM: MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amewataka wenyeviti wa mitaa na askari polisi wa ngazi ya kata kuimarisha ushirikiano katika kulinda amani na usalama ndani ya wilaya hiyo.
Mpogolo ameeleza hayo leo katika kikao kazi kilichowakutanisha Mkuu wa Wilaya, viongozi wa Polisi wa Mkoa na Wilaya ya Ilala, watendaji wa kata pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa kilichofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.
Kikao kazi hicho kililenga kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote ya Wilaya ya Ilala na kuhakikisha jamii inaendelea kuishi kwa amani na utulivu.

Akizungumza katika kikao hicho, Mpogolo amesema kuwa usalama wa wananchi unaanzia katika ngazi ya mtaa, hivyo ni wajibu wa viongozi kufanya kazi kwa umoja na mshikamano.
“Ulinzi na usalama unaanzia kwenye mtaa, hivyo ushirikiano wenu ndiyo nguzo ya amani ya wilaya yetu,” amesema Mpogolo.
Pia aliwataka viongozi hao kuwa walezi wa vijana, hususani waendesha bodaboda na wamachinga, akisisitiza kuwa ni kundi muhimu katika shughuli za kiuchumi na kijamii za kila siku, hivyo vijana hao wanahitaji mwongozo na ushirikiano ili wawe chachu ya maendeleo, si chanzo cha hatari.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, alimuhakikishia Mpogolo kuwa miundombinu yote ya serikali iliyoharibiwa baada ya Uchaguzi Mkuu inaendelea kukarabatiwa ili huduma kwa wananchi zirudi katika hali yake ya kawaida.
Katika hatua nyingine alibainisha kuwa baadhi ya ofisi za serikali na vituo vya polisi vilipata uharibifu, hali iliyosababisha wananchi kukosa huduma muhimu kwa muda.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kipolisi Ilala (RPC) Mgonja aliwahimiza wananchi kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu au vitendo vinavyohatarisha usalama katika maeneo yao, akisema taarifa zao ni ngao muhimu katika kulinda amani ya mtaa.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com