DAR ES SALAAM; Msanii wa muziki Khery Sameer ‘Mr Blue’ ameweka wazi kuwa mke wake ndie aliemsaidia kuacha kutumia madawa ya kulevya.
Akifanya mahojiano na BBC Mr Blue ambaye anatamba na kibao cha Mapozi amesema safari yake ya maisha na muziki kipindi anaanza muziki walitokea watu ambao ndio ilikuwa chanzo cha yeye kudondoka kimuziki kutokana na starehe.
.”Familia yangu ndio chanzo kikubwa cha kurudi kwenye ramani kwani niligundua kuwa nimeshaingia kwenye majukumu ya kifamilia.
“Mke wangu namshukuru sana kwani yeye ndiye amechangia kwa kiasi kikubwa mimi kubadilika, alikuwa ananiambia taratibu vitu vya kufanya na baadae aliposhika ujauzito ndio nikagundua naenda kuwa na familia”amesema
Pia ameongeza kuwa marafiki na watu walionizinguka ndio walinimpotosha kuwa na makundi yaliopelekea akaingia kwenye unywaji wa pombe na madawa.
“Mimi wakati naanza muziki nilikuwa mtoto na sikuwa na rafiki lakini watu walikuja wakijifanya wananijua wamesoma na mimi kwahiyo ule ushikaji mtu akichoma na mimi nachoma mara pombe nikawa siendi studio, nimeharibiwa na watu waliokuja baada ya mimi kuwa maarufu nashukuru Mungu na mke wangu nimerudi kwenye mstari”amesema Mr Blue