Mr Nice: Nilianza kushika pesa kabla ya kuimba

MWANZILISHI wa muziki wa Takeu, Lucas Mkenda maarufu Mr. Nice amesema sanaa ya uchoraji ndiyo iliyoanza kumuingizia fedha nyingi kabla hajaingia kwenye muziki na kuwa maarufu.

Mr. Nice amesema mashabiki wake wengi wanadhani alianza kushika fedha nyingi alipokuwa mwanamuziki lakini hawafahamu kama alikuwa na maisha mazuri kabla ya kuingia kwenye muziki.

“Watu wengi wanasema nimefulia kwa sababu hawanijui wanasema nimetumia vibaya fedha sasa walitaka nitumiaje? Nilitumia nilichokuwa nikiigiza na pia muziki ilikuwa sehemu nyingine ya mimi kupata fedha lakini kabla ha muziki nilikuwa nachora na kuuza picha kwa wazungu zilikuwa zikinipatia fedha nyingi lakini pia nilikiwa nikiuza duka la la mama hivyo nashika fedha nyingi wengi hawajui,” ameeleza Mr Nice.

“Nikweli muziki umeniingizia fedha nyingi lakini kabla sijaingia kwenye muziki nilikiwa na kazi nyingine nyingi zilizoniingizia fedha nyingi hivyo kutumia kwa starehe ilikuwa kawaida kwangu kwa kuwa nilikuwa na fedha kabla na nilipoingia katika muziki pia nikawa naingiza fedha nyingi zaidi,” amesema Mr. Nice.

Mr Nice enzi za umaarufu wake muziki wake uliwahi kuuza kopi zaidi ya milioni moja kiasi ambacho ni kikubwa kuwahi kutokea katika muziki nchini.

Habari Zifananazo

Back to top button