Mradi kuzalisha ajira 30,000

MRADI wa kongani ya kisasa ya viwanda (modern Indutrial park) inayoendelea kujengwa inapanga kujenga viwanda 202 vikitoa ajira ya moja kwa moja zipatazo 30,000.

Mradi huo unajengwa katika eneo la ukubwa wa ekari 1077 ambalo limegawanyika katika viwanja 210, kati ya hivyo viwanja 202 ni kwa ajili ya viwanda, vituo vya umeme viwili, maeneo ya biashara mawili, huduma za jamii tatu, bandari kavu moja na mitandao ya barabara.

Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Ashatu Kijaji alisema hayo jana mara alipotembelea eneo la mradi huo katika eneo la Disunyara na kikongo, Mlandizi wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.

Advertisement

Alisema Tanzania iliamua isiachwe nyuma na mapinduzi ya nne na kuelekeza nguvu katika maendeleo ya viwanda ili kujenga nchi katika nyanja mbalimbali.

Alisema hata katika dira ya maendeleo ya Taifa inayoishia mwaka 2025 imeelekeza kuwe na viwanda na katika kutekeleza hilo, katika kongani hiyo inauwezo wa kuajiri idadi kubwa ya wananchi lakini pia kuwa na uwekezaji mkubwa nchini.

“Tumeunganisha jitihada kuhakikisha malengo yanatimia na tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa utayari wake ulioonesha kuwa ujenzi wa uchumi nchi upo mikononi mwa sekta binafsi,” alisema Dk Kijaji na kuongeza kuwa mwekezaji wa mradi huo ni Kamaka Company Limited wa Dar es Salaam akishirikiana na serikali a Tanzania.

Hata hivyo alimpongeza mwekezaji huyo kwa utayari wake wa uwekezaji na kwamba lengo ni ili sekta binafsi iwezekushika uchumi wa nchi.

Alisema kupitia uwekezaji huo malengo ya vijana milioni moja wanaohitimu katika vyuo mbalimbali wanaweza kufikiwa kwa ajira na serikali iko tayari kushirikiana ili malengo ya uwekezaji huo yaweze kufanikiwa.

Akisoma taarifa ya mradi, Mkurugenzi Mtendaji wa mradi huo Charles Bilinga alisema makadirio ya awali yanaonesha kuwa ajira zisizopungua 200,000 zitatokana na uwekezaji huo wa viwanda kwa wakazi wa maeneo ya jirani na kongani.

Alisema ajira za moja kwa moja pindi mradi utakapokamilika zinakadiriwa kufikia 30,000 na pia wezesha kuongezeka kwa pato la taifa kupitia kodi mbalimbali shughuli za uzalishaji wa bidhaa na malighafi.

Bilinga alisema gharama za mradi huo hadi kukamilika ni sh trilioni 3 na bilioni 500 na kati ya fedha hizo Sh bilioni 122 na milioni 400 zitatumika kujenga miundombinu yote ndani ya kipindi cha miaka mitano nahadi sasa kiasi cha sh bilioni 35 zimetukima kwa ujenzi w amiundombinu.

Alisema mradi ulianza kutekelezwa Oktoba 2021 na klwa sasa unahusisha ujenzi wa lango kuu na uzio kuzunguka eneo lote la kongani ya viwanda lenye urefu wa takriban kilomita tisa ili kulinda usalama wa Kongani, ujenzi wa kituo cha polisi, jingo la utawala, jingo la ofisi na jengo la makazi ya wafanyakzi wa zimamoto, zahanati na kituo cha umeme wa megawati 54.

Kwa upande wake Ofisa Fedha na Masoko wa mradi huo, Tumaini Kabengula alisema mpaka sasa kuna mikataba 10 ya ununuzi wa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa viwanda,kuna viwanja 24 vilivyoshikiliwa vikisubiri kusainiwa kwa mkataba, wawekezaji watatu wamekwishaanza hatua za awali za ujenzi na wengine watano waliosaini mikataba wataanza mwaka huu.

Alisema wawekezaji waliotembelea kongani kwa nia ya kuwekeza ni 58 wakitokea India China, Urutuki, Sudan ya Kusini, Afrika Kusini, Rwanda, Somalia, Tanzania, Pakistan, Yemeni, Zambia, Falme za Kiarabu, Misri, Uganda, Kenya na Canada.

/* */