Mradi shule ya Mwanangwa wakamilika

MRADI wa shule maalum ya wasichana Mwanangwa, Kata ya Mabuki wilayani Misungwi mkoani hapa umekamilika tayari kwa matumizi  kuanzia Januari mwakani.

Mradi huo unatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kuanzia Aprili mwaka jana kwa gharama zaidi ya Sh millioni  648.7 na unahusisha madarasa manne, bweni, bwalo na matundu 12 ya vyoo.

“Miundombinu hiyo yote imeshakamilika kwa asilimia 100.

Tumeongezewa zaidi ya Sh millioni 225 kwa ujenzi wa maabara ya bailojia na Kemia, pamoja na jengo la utawala.

“Majengo haya yatakamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu ili yaanze kutumika Januari,” amesema Mratibu TASAF Wilaya ya Misungwi, Gloria Buname.

Mwenyekiti wa Kijiji Mwanangwa, Leonard Bukombe, amesema kwa kuanzia, shule hiyo itachukua wanafunzi 80.

Amesema mojawapo ya faida ya mradi huo ni kuwapunguzia wanafunzi mwendo wa zaidi ya kilometa saba, wanazosafiri kufuata huduma za shule ya sekondari eneo la Mawe Matatu, nje ya Kata yao.

Habari Zifananazo

Back to top button