‘Mradi uzingatie mahitaji halisi ya walengwa’

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), limepanga kutekeleza mradi wa kilimo, mifugo, uvuvi, miundombinu na biashara kwa ajili ya jamii iliyohamishwa kutoka eneo la Likong’oko Manispaa ya Lindi kupisha utekelezaji wa mradi wa gesi asilia ya kusindika (LNG), mkoani Lindi.

Mradi huo umetambulishwa katika kikao cha viongozi na watendaji wa TPDC , kkampuni ya gesi na mafuta ya Equinor na Shell na Kampuni ya Ushauri na Usimamizi wa Mradi ya RSK kukutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainabu Telack ofisini kwake, aliyetaka mradi huo uzingatie mahitaji halisi ya walengwa.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Kampuni ya RSK Tanzania, Jesper Johnson amesema lengo la mradi huo (mradi wa kilimo, mifugo, uvuvi, miundombinu na biashara) ni kuhakikisha wanarudisha hali ya uchumi ya jamii iliyohamishwa kutoka eneo la mradi wa LNG.

 

Amesema kuwa mradi huo ni wa miaka mitatu na utaanza na kuwatambua walengwa na kutambua mahitaji yao kwenye shughuli za kilimo, mifugo, uvuvi, biashara na miundombinu ya maendeleo.

Katika mazungumzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Telack amewataka watekelezaji wa mradi huo kuzingatia mahitaji halisi ya walengwa ikiwemo wavuvi na shughuli za wa uvuvi, wakulima na maeneo yao ya uzalishaji.

Telack amesisitiza kuwa mradi huo utekelezwe kukamilifu na uwafikie walengwa wote bila kumuacha mnufaika hata mmoja.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x