Mradi wa maji Rorya, Tarime waiva

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amemkabidhi mkandarasi eneo la ujenzi wa mradi wa majisafi na usafi wa mazingira  Wilaya za Rorya na Tarime wenye gharama ya Sh bilioni 134.

Hafla ya kusaini mkataba na kumkabidhi mradi huo  imefanyika eneo la chanzo cha maji Mingwa katika Kijiji cha Nyangombe.

Akizungumza leo Septemba 10,2022   Aweso amesema katika kipindi cha muda mrefu wananchi wa wilaya za Rorya na Tarime, wamekuwa wakihangaikia upatikanaji wa maji safi na salama, wakati Ziwa Victoria lipo karibu yao na ni chanzo cha uhakika.

“Serikali  ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu imedhamiria kwa dhati kumtua mama ndio,” amesema

Aweso amewataka wakandarasi kufanya kazi kwa weledi, uhakika, kasi na viwango kwani wananchi wamekwisha kuteseka kwa muda mrefu na mradi huo ni tumaini kubwa kwao na kwamba atawasimamia na kuwafuatilia mpaka mradi huo ukamilike hatua kwa hatua.

Habari Zifananazo

Back to top button