Mramba: Fungeni mfumo wa gesi kwenye magari yenu

SERIKALI imewataka wananchi wenye magari kugeukia mfumo wa nishati ya gesi kwa kufunga kwenye magari yao kwa kuwa unapunguza gharama kwa asilimia 40 ukilinganisha na Dizel na Petroli.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), kuhusu mafuta na gesi asilia uliofanyika katika Maonyesho ya 47 ya  Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) amesema utafiti uliofanyika unaonyesha matumzii ya nishati ya gesi kwenye  magari unapunguza garama kwa asilimia 40 ukilinganisha na  dezeli na petroli.

Mramba amesema kutokana na utafiti huo, serikali inawahamasisha watanzania kutumia zaidi gesi kwenye magari yao kwa kuwa dunia ndiko inakoelekea.

“Gesi asilia ni nishati safi na salama kwa magari ambapo bei yake iko chini ukilinganisha na petroli na humuwezesha dereva kutembea umbali mrefu kwa kutumia kiwango kidogo cha gesi.”Amesema Mramba na kuongeza

“Pia ni rafiki wa mazingira, kwa sababu haina  hewa ukaa ikilinganishwa na ile inayozalishwa na petroli inayosambaa angani na kusababisha ongezeko la joto na kuyeyuka kwa barafu, jambo linaloongeza kina cha bahari na kuathiri afya za watu na wanyama.”Amesema

Amesema kwa kutambua hilo, serikali inakaribisha sekta binafsi ziweze kushiriki katika mambo mawili makubwa.

“Moja  kujenga vituo vya kusambaza gesi kwenye magari na pili  kuanzisha karakana ya kubadilisha magari yanayotumia mafuta na gesi kwa pamoja. Kwa kufanya hivyo gharama za maisha ya watu wengi zitashuka.”Amesema

Amesema, Wizara wanalifanyia kazi jambo hilo kwa kuwa lengo ni kuona wananchi wengi wanatumia magari yenye mfumo wa gesi. Hivyo hivyo kwa majumbani gharama yake iwe  chini

Tanzania inakadiriwa kuwa na mita trilioni 230 za ujazo za gesi asilia, ingawa zilizothibitishwa mpaka sasa ni futi trilioni 57.5, hivyo kuiweka kwenye ramani ya dunia ikishika nafasi ya 82.

Gesi hiyo tayari imeanza kuchimbwa katika visiwa vya Songosongo wilayani Kilwa, mkoani Pwani na eneo la Msimbati mkoani Mtwara, ikitumika kuzalisha umeme na kuendesha mitambo ya baadhi ya viwanda nchini.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x