Mrema afariki dunia akiwa na miaka 77

Augustino Lyatonga Mrema

MWANASIASA Mkongwe na Mwenyekiti wa Chama cha TLP Bw. Augustino Lyatonga Mrema amefariki dunia leo Agosti 21 akiwa na umri wa miaka 77.

Mrema amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), kwa mujibu wa msemaji wa hospitali hiyo, Aminniel Eligaisha.

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole nakusema kifo hicho kimemsikitisha na kwamba atamkumbuka Mrema  kwa mchango wake katika mageuzi ya siasa, uzalendo na upendo kwa Watanzania. 

Advertisement

“Pole kwa familia na wana TLP. Mungu amweke mahali pema. Amen,” Ameandika Rais Samia.

Katika Kipindi cha uhai wake, Mrema aliyezaliwa Vunjo amewahi kuwa Mbunge, Waziri wa Mambo ya Ndani na aligombea kiti cha Urais mwaka 1995 kupitia chama cha NCCR-Mageuzi.  Mrema alikuwa pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Parole. 

1 comments

Comments are closed.