Kamwelu ajipanga kuwashika mkono wahitaji

DAR ES SALAAM: MUIGIZAJI maarufu nchini Nelly Kamwelu amesema baada ya kukamilisha mipango yake ya kazi ataona ni jinsi gani ataanza tena kurudisha kwa jamii na namna ya kuwafikia wenye uhitaji, muigizaji huyo ameiambia HabariLEO.

Mwigizaji huyo ambaye ni mhitimu wa chuo cha uigizaji cha New York Film Academy cha nchini Marekani amesema kurudisha kwa jamii ni muhimu kwake kama ambavyo ameshawahi kufanya hivyo miezi kadhaa iliyopita.

“Kuna miradi yangu miwili naipanga tumuombe Mungu kama kila kitu kitaenda sawa mwishoni mwa shughuli zangu nitalifanyia kazi hilo, nitalifanya miezi kadhaa ijayo,” amesema Kamwelu.

SOMA: Kampeni msaada wa kisheria yaanza Ludewa

Mshindi huyo wa taji la Miss Universe Tanzania 2011 amesema wakati akiwaza hilo kwa sasa hafikirii kuwa na taasisi itakayorudisha kwa jamii ila huenda mwakani akafikiria hilo.

“Sidhani kama nitakuwa na muda wa kuandaa ‘Foundation yoyote kwa sasa labda Mungu akipenda mwakani,” ameongeza Kamwelu.

Habari Zifananazo

Back to top button