Mrithi wa Makonda kujulikana leo

DAR ES SALAAM: kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imekutana leo katika Ikulu ya Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine itakuwa na jukumu la kujaza nafasi ya Katibu wa Itikadi, Uendezi na Mafunzo.

Uamuzi huo unatokana na Mwenyekiti wa Chama na Rais Samia Suluhu Hassan kumteua aliyekuwa mwenezi, Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Mbali na nafasi ya Mwenezi, pia kuna nafasi zingine tatu ambazo zimeachwa wazi baada ya Rais Samia kuwateua kushika nyadhifa mbalimbali. Nafasi hizo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Bara, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho katika

Advertisement

Fakii Lulandala aliyekuwa Katibu Mkuu UVCCM ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Gilbert Kalima aliyekuwa Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga. Anamringi Macha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) yeye aliteuliwa Machi 12 mwaka huu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na tayari alikwishaapishwa.

Wanaopigiwa ramli kurithi mikoba ya Makonda ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Kenani Kihongozi ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM.

Pia, yupo Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Antony Mtaka na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila. Wengine ni Amos Makalla aliyekuwa RC (Mwanza), Ally Hapi (Mara) na John Mongella (Arusha).