Msafara wa Makonda wapata ajali

TAARIFA iliyotufikia kwenye chumba chetu cha habari inaeleza kuwa msafara wa Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda umepata ajali katika eneo la Masasi mkoani Mtwara

Imeelezwa kuwa ajali hiyo imetokea alasiri ya leo katika msafara wa muenezi Makonda uliokuwa unatoka mkoani Ruvuma kuelekea jijini Dar es salaam

Kuna taarifa za baadhi ya watu kujeruhiwa na kukimbizwa katika Hospital ya Mkoa wa Mtwara na huku kukiwa hakuna kifo chochote.

Habari Zifananazo

Back to top button